Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Desderius John Mipata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. DESDERIUS J. MIPATA aliuliza:- Hapa nchini pamekuwepo na ongezeko kubwa la Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kifedha kama vile Benki, Vikundi mbalimbali kama VICOBA, Taasisi za Kukopesha Watumishi, Taasisi za kukopesha wafanyabiashara na wakati mwingine watu na mitaji yao wanakopesha watumishi (kienyeji) kwa kificho ficho:- (a) Je, ni chombo kipi hasa chenye wajibu wa kufuatia kodi zinazotozwa na wananchi? (b) Je, kodi zinazotozwa ni halali? (c) Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha wananchi wake hawaibiwi kwa njia hiyo?

Supplementary Question 1

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza:-
La kwanza; kwa kuwa wapo watu wanaokopesha
kienyeji na hutoza riba kubwa inayofikia asilimia 30 kwa mwezi na inapotokea mkopaji akakosa kulipa maana yake mwezi unaohusika gharama hiyo hupanda kwa maana ya compound interest kwamba mtaji pamoja na asilimia iliyopaswa kutozwa hufuata kwa mwezi mwingine na hali
hii huacha wananchi katika hali ngumu sana. Je, Serikali inawajua vizuri hawa watu na ina mpango gani wa kutafuta njia ya kuimaliza kadhia hii? (Makofi)
Swali la pili; kwa kuwa watumishi ndiyo walengwa
wakuu katika jambo hili pamoja na wastaafu ambao wako karibu kustaafu na kadhia hii huwafanya wapoteze hata ufanisi kazini; je, Serikali haioni umuhimu wa kulichukulia hili
jambo kama vita ya madawa ya kulevya kwa sababu watumishi wengi wanastaafu wakiwa hawana kitu chochote na familia zao zinasambaratika?

Name

Dr. Philip Isdor Mpango

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza katika jibu la msingi, ni kweli kabisa riba hizi kwa hawa wakopeshaji wa mitaani ni mzigo mkubwa kwa wale wanaolazimika kwenda kukopa huko
na ndiyo maana Serikali imekuwa inasisitiza kwamba kadri inavyowezekana wasiende huko, lakini jibu langu la msingi ni kwamba; sasa hivi Serikali tunafanya jitihada kubwa na tayari tumeshaandaa Waraka wa Baraza la Mawaziri ili jambo hili baada ya kulifanyia kazi kwa mapana yake liweze kushughulikiwa kwa ukamilifu na maagizo maalum ya Serikali baada ya kuwa waraka huu umepitiwa na Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, lile la kusema kwamba
tuichukulie kama vita nafikiri tusiende huko kwa sasa kwa sababu waraka umeandaliwa, ni vizuri tupate nafasi ya kulichukulia maamuzi tukiwa tumetulia. Ahsante.