Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:- Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malalamiko baina ya wakulima na Mamlaka ya Mapori ya Hifadhi ya Misitu, kwa sababu ya kuongezeka kwa watu lakini ardhi haiongezeki, hivyo kufanya ongezeko hili la watu wakose ardhi kwa shughuli zao za kilimo na mambo mengine yahusuyo ardhi:- Je, ni lini Serikali italeta Bungeni Muswada wa Sheria husika ili kufanya marekebisho katika mipaka ya Hifadhi hizo ili kupata eneo la kilimo kwa wananchi walioongezeka ambao hawana maeneo ya kilimo.

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa, wananchi wanaoingia kwenye hifadhi ya misitu siyo kwamba wanaingia kwa sababu ya ukatili ni kwa sababu ya kukosa maeneo ya kuishi na kulima.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano; wananchi wa Wilaya ya Kasulu wanaoingia kwenye pori ya Hifadhi ya Kagerankanda ni kwa sababu watu wameongezeka, ardhi ni ile ile, maeneo ya kilimo yamekuwa ni kidogo. Je, kwa nini, Serikali isiwaruhusu waendelee kulima wakati Serikali inaandaa utaratibu mwingine wa kupima mipaka. (Makofi)
Swali la pili; kwa kuwa, ongezeko la watu ni kubwa sana, kwa nini, Serikali isitenge baadhi ya maeneo ya misitu ili wananchi waruhusiwe kuishi na kuwapunguzia tatizo hili la kuhangaika kutafuta maeneo ya kulima?
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Name

Prof. Jumanne Abdallah Maghembe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Answer

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba wako wananchi ambao wameingia na wamejenga ndani ya maeneo ya misitu na wanakaa humo kufanya shughuli za kibinadamu. Sheria zetu za nchi zinakataza wananchi kuingia na kujenga, kulima ndani ya hifadhi zetu. Kwa hiyo, naomba niwahamasishe wananchi hawa wafuate sheria na wafuate sheria bila shuruti. Kwa hiyo, waondoke kwenye maeneo ya hifadhi na washirikiane na Halmashauri pamoja na Serikali za vijiji vyao kuwapangia maeneo mengine ya kuishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ongezeko la watu ni phenomena ambayo inatokea dunia nzima. Siyo jambo la Tanzania peke yao, kama ambavyo mmeona, nchi ambazo zinaendelea na zile ambazo zimeshaendelea, idadi ya wakulima inaendelea kupungua mpaka kufikia asilimia 20 katika nchi nyingi za Ulaya au kule Marekani, hii inatokana na watu kufanyakazi zingine, siyo lazima wote tuwe wakulima, kufanya kazi zingine ambazo mahitaji yake ya ardhi ni madogo kama vile ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki kuanzisha viwanda vidogovidogo kama nilivyoeleza kwenye swali langu la msingi ili kuhakikisha kwamba maisha yetu yanaendelea, lakini na misitu yetu inakuwepo ili maisha yetu yaendelee kwa ustaarabu ambao unatakikana.