Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Majosho kwenye Vijiji vya Gwandi na Takwa – Chemba?

Supplementary Question 1

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi. Kwanza kabisa, naomba nichukue fursa hii kuishukuru Wizara kwa majosho matano. Nina swali moja tu la nyongeza. Nataka kujua kama Wizara inajua kwa uhakika katika vijiji vyetu vyote 114, mahitaji ya majosho ni kwa kiwango gani, ahsante.

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ni kweli kwamba Wizara ina Database ya kujua wapi panahitajika josho lipi, kwa size gani na kwa umuhimu gani? Pia, Mheshimiwa Mbunge kama anaona kuna sehemu ambapo sisi kama Serikali tunapaswa kwenda kujenga josho, alete taarifa zake tuweze kufanyia kazi kwenye maeneo hayo. Hata hivyo, mpaka sasa database ya vijiji ambavyo majosho yanatakiwa kujengwa, Serikali ina hiyo database, ahsante. (Makofi)