Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 4 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 65 2024-02-02

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Majosho kwenye Vijiji vya Gwandi na Takwa – Chemba?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Lujuo Monni, Mbunge wa Chemba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa majosho nchini ili kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na kupe na wadudu wengine. Kupitia mpango huo, jumla ya majosho mapya 747 yamejengwa kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2020/2021 hadi Juni, 2023 yakiwemo majosho matano yaliyojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba katika Vijiji vya Tumbakose, Mlogia, Mondo, Msaada na Masimba ambapo ujenzi umekamilika na yameshaanza kufanya kazi.

Mheshimiwa Sipika, kwa kutambua umuhimu wa majosho katika kudhibiti magonjwa ya mifugo nchini, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali itaendelea kutenga fedha za ujenzi wa majosho maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya Vijiji vya Gwandi na Takwa.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.