Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Watanzania wote wanajua kusoma na kuandika?

Supplementary Question 1

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu ya Serikali; pamoja na majibu ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

(a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwabaini wale watanzania wenye umri wa zaidi ya miaka 35 ambao hawako katika programu ya Re-Entry na zile programu afua zingine wasiojua kusoma na kuandika ili waweze kufikiwa?

(b) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikishwa kwamba, shule za msingi na shule za sekondari zote zinakuwa na maktaba ili kusudi wanafunzi waweze kujisomea?)

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza la Mheshimiwa Toufiq, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha kueleza katika majibu ya swali la msingi. Serikali inazo kwanza takwimu za kutoka NBS zinazotuthibitishia uwepo wa watu wasiojua kusoma na kuadika. Ongezeko hili la watu wasiojua kusoma na kuandika limekuwa likipungua kutoka asilimia 78 mwaka 2012, mpaka asilimia 83 katika Sensa ya mwaka 2022.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo naomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa vile tayari sasa tunafahamu idadi hii au takwimu hizi, Serikali kupitia mpango mikakati hii ambayo nimeitaja ikiwemo na mpango wa Serikali wa Uwiano katika Elimu ya Watu Wazima na Jamii unaojulikanika kama MKEJA, ndio ambao utahakikisha sasa idadi hii ya Watanznaia wasiojua kusoma na kuandika, wale wenye umri zaidi wa miaka 35 tunaweza kuwafikia.

Mheshimiwa Spika, pia katika eneo la pili la suala la shule zetu za msingi na sekondari kuwa na maktaba, suala hili tayari Serikali imeshalifanyia kazi. Katika miundombinu ambayo inajengwa sasa hivi katika Shule zetu za msingi pamoja na sekondari ni lazima kuwe na jengo la maktaba, nakushukuru sana.

Name

Rose Cyprian Tweve

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Watanzania wote wanajua kusoma na kuandika?

Supplementary Question 2

MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Spika, kwa maelezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri tuna zaidi ya asilimia 16 ya Watanzania ambao hawajui kusoma na kuandika. Sasa nilitaka kujua Mkakati wa Serikali wa kuhakikisha tunatenga bajeti kwenda kuhudumia Watanzania ambao wanapata elimu kutoka kwenye mfumo usio rasmi kama vile, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ambao kwa sasa hawapati ruzuku, nakushukuru sana.

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante na naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Tweve, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Tweve anatoa ushauri kwamba, Serikali tuweze kupanga bajeti kupitia Taasisi yetu ya Elimu ya Watu Wazima. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa, tutakwenda kufanya tathmini ya kina namna gani tunaweza kutenga bajeti kwenye Taasisi yetu ya Elimu ya Watu Wazima, ili kuweza kulifikia kundi hili la watu wasiojua kusoma na kuandika.

Name

Najma Murtaza Giga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Watanzania wote wanajua kusoma na kuandika?

Supplementary Question 3

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwa na takwimu hizo za wasiojua kusoma na kuandika pamoja na mikakati mizuri ya Serikali, je, Serikali haioni umuhimu sasa wa kuwa na takwimu halisi za viwango vya elimu na makada zake, kuanzia kiwango cha juu cha elimu hadi kufikia chini kwa mustakabali mzuri wa maendeleo ya Taifa letu?

Name

Prof. Adolf Faustine Mkenda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rombo

Answer

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwanza namshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu mazuri sana aliyoyatoa, ningeomba nitoe maelezo kidogo kuhusu suala la takwimu kwa Mheshimiwa Najma.

Mheshimiwa Spika, tunao mfumo wa takwimu wa elimu unaitwa BEST (Basic Education Statistics of Tanzania) ambao kwa muda mrefu ulikuwa uki-focus kwenye shule ambazo zinamilikiwa na TAMISEMI na shule zinazotumia mtaala wa Taifa. Sasa hivi tunacho kikosi kazi kinafanya kazi kuhakikisha kwamba, kuna dawati la kuhakikisha kwamba, takwimu za elimu kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu zinakusanywa katika document ambayo tutakuwa tunaitoa kila mwaka.

Mheshimiwa Spika, vilevile tutajumuisha watoto wanaosoma katika hizi shule zingine ambazo zinatumia mitaala kama Cambridge. Kazi hiyo inaendelea na hata leo mchana tunakutana kwa ajili ya kazi hiyo. Kwa hiyo, tunaelewa kabisa concern ya Mheshimiwa Najma na tunaifanyia kazi. (Makofi)

Name

Martha Festo Mariki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Watanzania wote wanajua kusoma na kuandika?

Supplementary Question 4

MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Serikali, upi sasa mkakati wa haraka zaidi kuhakikisha tunawanusuru watoto wadogo ambao wanapatikana hususan katika jamii za wafugaji na wavuvi ambao hawajui kabisa kusoma na kuandika, kuweza kuwanusuru watoto hao ili waweze kujua kusoma na kuandika?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Martha, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika maboresho ya mtaala ambayo tuliyapitisha mwaka jana, unakwenda kuchukua ngazi zote za watoto wetu kuhakikisha kwamba wanakuwa shule. Katika sera pamoja na mitaala hii ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha kwamba, yule mtoto ambaye tayari ameshafika umri wa kwenda shule aweze kwenda shule.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, nitoe tu maelekezo kwa Wakurugenzi wetu wote wa halmashauri, Wakuu wa Wilaya ambako ndiko hawa watoto waliko, iwe eneo la wafugaji au iwe eneo la wavuvi, kuhakikisha vijana wetu ambao tayari wameshafikia umri wa kwenda shule waweze kuandikishwa na kuweza kukaa shuleni kwa ajili ya kusoma, nakushukuru.