Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ng'wasi Damas Kamani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NG’WASI D. KAMANI K.n.y. MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa idhini kwa Makampuni binafsi kutoa elimu ya kujikinga na majanga ya moto kwa Wananchi na Taasisi nchini?

Supplementary Question 1

MHE. NG’WASI D. KAMANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali na pamoja na kwamba focus ya Serikali sasa hivi ni kufanya kazi na sekta binafsi kwa mfumo wa PPP. Je, ni lini sasa uhuishwaji huu wa hizi kanuni utakamilika ili kuweza kuwezesha sekta binafsi kuingia na kutoa elimu ya majanga haya?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa madhumuni ya kuharakisha hili jambo ambalo amelipendekeza Mheshimiwa Kamani, ni jambo jepesi kwa sababu Kanuni zinaishia kwa Mheshimiwa Waziri. Kwa hiyo, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wataandaa mapendekezo ya namna ya kuzingatia kwenye Kanuni zilizopo ili kuhuisha na kujumuisha hili suala kwenye utendaji wa Zimamoto na Uokozi, nashukuru.