Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Esther Edwin Maleko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESHTER E. MALLEKO aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kuhusisha Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika kulinda miradi mikubwa ya kimkakati?

Supplementary Question 1

MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina swali moja la nyongeza. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuongeza au kuajiri vijana wengi zaidi na kuwapa mafunzo hayo ili waweze kusimamia ile miradi mikubwa inayotolewa kwenye mikoa na wilaya, kwa sababu mingi imeonekana ikihujumiwa sana? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI K.n.y. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa madhumuni kama aliyoyaeleza Mheshimiwa Mbunge Malleko, ni kweli kwamba Serikali ina dhamira na imekuwa ikiajiri vijana kwa ajili ya kujiunga na vyombo vyetu vingi vya usalama ikiwemo Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi, Fire na Uokozi pamoja na Magereza.

Mheshimiwa Naibu Spika, vyombo vyote hivi hushiriki katika shughuli za ulinzi na usalama wa miundombinu inayoendelezwa kwenye maeneo yetu kupitia Kamati za Usalama za Wilaya na Kamati za Usalama za Mikoa, nashukuru.