Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hassan Seleman Mtenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Primary Question

MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itazilipa fedha Kampuni za Usambazaji wa Mbolea na Viuatilifu Mtwara?

Supplementary Question 1

MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nina swali moja la nyongeza;

Je, ni lini mfuko wa pembejeo utarejeshwa ili Serikali iweze kumaliza haya matatizo yote ya ulipaji wa madeni ya watu ambao wanaleta mbolea?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nimjibu Mheshimiwa Mbunge kwamba, jambo hili liko katika mchakato na sisi kama Wizara ya Kilimo tunalipitia upya ili kuhakikisha tunaondokana na hizi changamoto, kwa hiyo tutakapolimaliza tu, tutalirudisha kwa wananchi mara moja kama ilivyokuwa hapo awali ili kuondokana na kero hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo jambo hili tumelipokea.