Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itagawa Kata za Matiri, Litumbandyosi, Linda, Mkumbi, Litembo, Nyoni, Maguu na Langiro Wilayani Mbinga?

Supplementary Question 1

MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na nia hii ya kugawa kata tuna nia pia ya kugawa vijiji na mwaka unaokuja ni mwaka wa uchaguzi. Je, Serikali inatoa kauli gani kwa Halmasahuri ya Wilaya ya Mbinga ambayo vijiji vingi vimeleta maombi ya kugawanywa.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kauli ya Serikali ni kwamba taratibu za kisheria za maombi ziendelee, na Serikali itapokea maombi hayo kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, itafanya tathimini ya vigezo lakini kipaumbele cha kwanza kwa sasa ni kuboresha kwanza maeneo ya kiutawala yaliyopo. Lakini hili halizuii kuendelea na taratibu katika ngazi ya halmasahuri, ahsante. (Makofi)