Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 37 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 482 2023-05-31

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:-

Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya ujenzi wa daraja la juu katika Mto Mwamanongu?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Leah Jeremiah Komanya, Mbunge wa Jimbo la Meatu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilitenga fedha kiasi cha shilingi milioni 43 kwa ajili kufanya usanifu wa Daraja la Mto Mwamanongu. Usanifu huo umekamilika na jumla ya shilingi bilioni 7.5 zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo. Serikali itajenga daraja hilo kadri ya upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuhudumia miundombinu ya Wilaya ya Meatu kwa kujenga, kukarabati na kufanya matengenezo ya barabara na madaraja kulingana na upatikanaji wa fedha.