Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 9 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 130 2023-09-08

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:-

Je, lini huduma ya Mawasiliano ya Simu itapelekwa Kata za Bwawani, Oldonyowas, Laroi, Mwandet, Oljoro na Oldonyosambu?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Noah Saputu, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) itafanya tathmini ili kubaini changamoto ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika Kata za Bwawani, Oldonyowas, Laroi, Mwandet, Oljoro na Oldonyosambu zilizopo Jimbo la Arumeru Magharibi, tathmini hii itasaidia kufahamu ukubwa wa tatizo na mahitaji halisi ili hatimaye yaweze kuingizwa katika orodha ya miradi itakayotekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha na kutangazwa katika zabuni zijazo, ahsante.