Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 78 2023-09-05

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga barabara ya mchepuo kwenda Moshi kupitia Chekereni – Kahe – Mabogini - TPC kwa kiwango cha lami?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Charles Stephen Kimei, Mbunge wa Jimbo la Vunjo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii iko kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 kujengwa kwa kiwango cha lami. Hadi sasa TARURA Mkoa wa Kilimanjaro imefanya usanifu wa barabara yote kilometa 31.25 ambapo kwa kuanzia makisio ya ujenzi wa kilomita 12 kwa kiwango cha lami yenye jumla ya shilingi bilioni 15 yamewasilishwa TARURA makao makuu kwa hatua zaidi.