Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 5 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 72 2023-09-04

Name

Godwin Emmanuel Kunambi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlimba

Primary Question

MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani kuhusu ujenzi wa barabara ya Mafinga hadi Mlimba?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, nami kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusimama mbele ya Bunge lako kama Naibu Waziri wa Ujenzi, naomba nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, maana ametoa kibali hiki. Nichukue fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini ili niweze kumsaidia katika nafasi ya Unaibu Waziri wa Ujenzi, pia nikuahidi kwamba nitatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba sasa nijibu swali. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Godwin Emmanuel Kunambi, Mbunge wa Mlimba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara inayoanzia Mafinga, eneo la Kinyanambo ā€˜Cā€™ hadi Kihansi (Mlimba) yenye urefu wa kilometa 126.39, ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024 jumla ya milioni 250 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo. Baada ya kukamilika usanifu na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.