Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 2 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 33 2023-08-30

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha inapata data za bidhaa zote za kilimo zinazosafirishwa nje ya nchi?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Grace Victor Tendega, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inaendelea kuboresha mfumo wa Agricultural Trade Management Information System (ATMIS) kwa ajili ya kuufungamanisha na mfumo wa pamoja wa forodha wa Tanzania (Tanzania Custom Intergrated Systems - TANCIS) wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kufunganishwa kwa mfumo wa ATMIS na TANCIS kutaboresha upatikanaji wa takwimu za mazao na bidhaa za kilimo zinazoingizwa au zinazosafirishwa nje ya nchi.