Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 2 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 32 2023-08-30

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza: -

Je, lini Serikali itafufua kilimo cha pamba katika Wilaya ya Kilwa?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Francis Kumba Ndulane, Mbunge wa Kilwa Kaskazini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa maeneo yaliyo chini ya karantini ya pamba katika eneo la kusini mwa Tanzania kutokana na uwepo au kupakana na nchi zilizoathiriwa na funza mwekundu (diparopsis castenea) ambaye ni mdudu hatari wa zao la pamba.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2020/2021 Serikali ilifanya tathmini ya hali ya funza mwekundu na kubaini kuwa mdudu huyo bado yupo katika maeneo ya karantini. Aidha, Wizara itaendelea kufanya utafiti kwa kushirikiana na Taasisi za Kimataifa kuhusu namna bora ya kudhibiti mdudu huyo.