Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 22 2023-08-30

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Songambele ili kupunguza msongamano kwenye Kituo cha Afya Nkwenda Wilayani Kyerwa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Sebba Bilakwate, Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha wa 2021/2022, Serikali ilitenga bajeti ya shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Rutunguru katika Tarafa ya Kaisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya kwenye Kata za kimkakati kote nchini ikiwemo Kata ya Songambele iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, ahsante. (Makofi)