Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 31 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 414 2023-05-23

Name

Muharami Shabani Mkenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza: -

Je, lini Serikali itaongeza eneo na kuboresha Skimu ya Umwagiliaji ya Mto Ruvu – Bagamoyo?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Muharami Shabani Mkenge, Mbunge wa Bagamoyo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Skimu ya Kisere ambayo ni miongoni mwa skimu katika bonde la mto Ruvu. Aidha, Serikali inaendelea na hatua mbalimbali za kubaini maeneo yanayofaa kwa ujenzi wa mabwawa ili kuhudumia skimu zilizopo katika bonde hili, kwani hii itaepusha changamoto ya ukosefu wa maji kwa wakulima kwa kuwa Mto Ruvu unategemewa kwa matumizi mbalimbali ikiwemo matumizi ya majumbani kwa wakazi wa ukanda wa Pwani na Dar es Salaam.