Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 31 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 402 2023-05-23

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Primary Question

MHE. DEUS C. SANGU aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati Kituo cha Afya cha Msanda Muungano katika Tarafa ya Mpui?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, 0FISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa kukarabati vituo vya afya vikongwe nchini kikiwemo Kituo cha Afya Msanda Muungano kwa kutenga bajeti kwa ajili ya kuongezea miundombinu ili kuviwezesha kutoa huduma muhimu ikiwemo upasuaji wa dharura kwa mama wajawazito.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya Afya ikiwemo kituo cha Msanda Muungano katika Tarafa ya Mpui.