Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 3 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 47 2023-02-02

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itafanya kilimo kuwa kipaumbele cha kwanza cha Taifa kwa kupunguza bei ya mbolea?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo napenda kujibu swali la Mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto ya kupanda kwa bei ya mbolea katika msimu wa mwaka 2020/2021. Katika kukabiliana na changamoto hiyo, msimu wa mwaka 2022/2023 Serikali inatekeleza mpango wa utoaji wa mbolea za ruzuku kwa wakulima ili kuwaongezea uwezo wa kununua na kutumia mbolea. Hadi kufikia tarehe 31 Januari, 2023 jumla ya tani 246,714 za mbolea zimenunuliwa na wakulima kwa bei ya ruzuku ikilinganishwa na tani 173,957 za mbolea ambazo zilinunuliwa katika kipindi cha mwezi Julai hadi Januari, 2021.