Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 15 Sitting 23 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 189 2019-05-08

Name

Augustino Manyanda Masele

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. AUGUSTINO M. MASELE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbogwe?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Augustino Manyanda Masele, Mbunge wa Mbogwe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali ilitoa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali 67 za Halmashauri. Aidha, katika mwaka wa fedha 2019/2020 Serikali imetenga shilingi bilioni 23.9 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 52 na Hospitali 27 za Wilaya. Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ni miongoni mwa Hospitali hizo 27 na imetengewa shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.