Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 2 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 25 2023-11-01

Name

Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Chuo cha VETA Wilayani Kakonko?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aloyce John Kamamba, Mbunge wa Jimbo la Buyungu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inayo azma ya kujenga Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika kila mkoa na wilaya nchini. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kujenga Vyuo vya VETA katika wilaya 64 ambazo zilikuwa hazijajengewa vyuo hivyo. Aidha, Wilaya ya Kakonko ni miongoni mwa wilaya hizo 64 ambazo zinajengewa vyuo hivyo.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali imeshapeleka kiasi cha shilingi 228,000,000 pamoja na vifaa vya ujenzi ikiwemo nondo na sementi kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Kakonko ambapo ujenzi upo katika hatua ya kujenga misingi ya majengo. Ahsante sana.