Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 6 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 86 2023-11-06

Name

Iddi Kassim Iddi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Primary Question

MHE. IDDI K. IDDI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga minara ya simu katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Msalala?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, Mbunge wa Jimbo la Msalala, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imepata mtoa huduma wa kufikisha huduma za mawasiliano katika Kata ya Ntobo yalipo Makao Makuu ya Halmashauri ya Msalala. Kampuni ya Simu ya Vodacom ndiyo ilishinda zabuni ya kujenga mnara huo kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa Vodacom inaendelea na hatua mbalimbali za utekelezaji wa ujenzi wa mnara huo.