Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 6 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 76 2023-11-06

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kutumia eneo la uwekezaji la Kisasiga – Bukene kutengeneza miundombinu ya Block Farms kwa kilimo cha alizeti?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Selemani Jumanne Zedi, Mbunge wa Jimbo la Bukene kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imepanga kutambua na kupima mashamba makubwa mapya 30 yenye jumla ya hekta 200,000 kwa ajili ya uwekezaji likiwemo eneo la uwekezaji la Kisasiga-Bukene, Wilayani Nzega.

Mheshimiwa Spika, eneo la uwekezaji la Kisasiga-Bukene lina jumla ya ekari 48,000 zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za uwekezaji. Aidha, Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo iliungana na Watalaam wa Halmashauri ya Nzega kufaya upembuzi wa awali pamoja na tathmini ya kina ya udongo katika eneo hilo ili kupata taarifa za kina za afya ya udongo iwapo eneo hilo linafaa kwa kilimo cha Alizeti pamoja na kutengenezwa miundombinu ya Block Farms.