Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 70 2023-11-06

Name

Joseph Anania Tadayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:-

Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais ya ujenzi wa Stendi ya kisasa katika Mji wa Mwanga?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Anania Tadayo, Mbunge wa Jimbo la Mwanga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto ya ufinyu wa stendi ya magari katika Halmashauri ya Mwanga. Halmashuri imeandaa andiko lenye thamani ya shillingi bilioni 3.2 kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya kisasa na kuliwasilisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI mwezi Agosti, 2023 ambapo wataalam wanaendelea na mapitio ya andiko hilo kulingana na vigezo kwa ajili ya utekelezaji, ahsante.