Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 42 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 368 2022-06-10

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka mtaalam wa X–Ray katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Minza Simon Mjika, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022 inaajiri watumishi 7,612 wa kada mbalimbali za afya, wakiwemo wataalam wa X-Ray. Hivyo, Hospitali ya Wilaya ya Meatu itapatiwa mtaalam wa X-ray baada ya taratibu za ajira kukamilika, ahsante.