Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 39 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 343 2022-06-07

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: -

Je, Serikali haioni haja ya kuipandisha hadhi Zahanati ya Kijiji cha Sojo ili kiwe Kituo cha Afya na kuweza kuhudumia wananchi na watumishi wa Mradi wa Bomba la Mafuta?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Selemani Jummane Zedi, Mbunge wa Jimbo la Bukene kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Sojo ni moja kati ya vijiji saba vya Kata ya Igusule yenye wakazi 23,237. Kata hii ina zahanati moja iliyopo katika Kijiji cha Sojo ambayo inaendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kwenye Kata ya Igusule.