Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 37 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 334 2022-06-03

Name

Dr. Jasson Samson Rweikiza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza: -

Je, ni lini ujenzi wa Chuo cha VETA Burugo – Nyakato katika Jimbo la Bukoba Vijijini utakamilika?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante; kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Jasson Samson Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera ambacho ujenzi wake ulianza mwaka 2019. Utekelezaji wa mradi huo unafanywa kupitia ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China wenye thamani ya shilingi bilioni 22.4 na mradi umefikia asilimia 96 na unategemea kukamilika mwezi Juni, 2022.

Mheshimiwa Spika, kukamilika kwa mradi huo kutatoa fursa ya utoaji wa mafunzo kwa wananchi wa Jimbo la Bukoba Vijijini na Mkoa wa Kagera kwa ujumla. Nakushukuru.