Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 37 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 332 2022-06-03

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza: -

Je, nyumba bora ya kuishi inatakiwa kuwa na sifa zipi na ni kwa nini Serikali haiweki ruzuku kwenye vifaa vya ujenzi?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naomba kumjibu Mheshimiwa Joseph George Kakunda, Mbunge wa Sikonge na Chifu wa Wakonongo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nyumba ni mojawapo ya mahitaji muhimu ya mwanadamu. Nyumba bora ni ile yenye huduma bora kwa usalama na afya kwa wakazi wake. Jitihada za Serikali kuhakikisha nyumba bora zinajengwa kwa gharama nafuu ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha vifaa vya ujenzi, kufanya utafiti na kuwezesha matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kazi za ujenzi na kuhamasisha taasisi za fedha kutoa mikopo kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na ununuzi wa nyumba.