Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA Aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia ujenzi wa Jengo la Manispaa ya Tabora ambao umesimama kwa muda mrefu sasa huku shughuli za Manispaa zikiendelea kufanyika kwenye majengo ya zamani yaliyochakaa?

Supplementary Question 1

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimsahihishe kidogo Naibu Waziri majengo yale yalianza kujengwa mwaka 2012, mwaka 2015 majengo yalikuwa yameshasimama.

Mheshimiwa Spika, Serikali haioni umuhimu wa kutuongezea fedha badala ya bilioni moja ili tuweze kukamilisha majengo yale tuondokane na adha ya kufanyia vikao madiwani na watumishi kwenye maeneo vyumba vidogo sana ambavyo hata hewa nzuri havina. Majengo yale yameshakuwa ni ya muda mrefu mpaka yanatoa ule ukungu wa kijani Serikali haioni umuhimu wa kutuongezea fedha ili tuweze kumaliza kabisa majengo yale ili tuachane nao waendelee kwenye maeneo mengine? Nashukuru.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hawa Subira Mwaifunga, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mhesimiwa Spika, nchi yetu ni kubwa na kwenye jibu langu la msingi nimeongea namna ambavyo Serikali imeelekeza nguvu kubwa kwenye ujenzi wa majengo ya utawala kwenye halmashauri takribani 100 hivi sasa. Kwa hivyo, safari ni hatua tumeanza na bilioni na tutaendelea kadri ya fedha zainapopatikana tutakwenda kwa awamu kupeleka fedha hizo ili kukamilisha majengo hayo. Kwa hiyo, nimhakikishie kwamba ni kipaumbele cha Serikali na tutahakikisha tunakamilisha jengo hilo kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.