Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Serikali imekuwa na utaratibu wa kukarabati shule zake za sekondari na za msingi nchini:- Je, ni lini Serikali itafanyia ukarabati Shule za Sekondari Masagulu, Lwande, Mkuyu na Shule za Msingi Songe na Masagulu zilizopo Wilayani Kilindi?

Supplementary Question 1

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, kwanza nampongeza na niwapongeze TAMISEMI kwa kutupatia kiasi kilichotajwa kwa ajili ya shule zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kwamba Halmashauri zetu nyingi hazina uwezo wa mapato, lakini natambua dhamira ya Serikali ya kutoa elimu bure. Nina maswali mawili ya nyongeza:-

Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kukarabati shule kongwe ambazo ni za muda mrefu? Kwa mfano, Shule ya Msingi Masagali ya mwaka 1940 na Shule ya Msingi Songwe 1952? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kutembelea hizi ili ajionee hali halisi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA C. WAITARA):
Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Kigua kwa kazi nzuri ambayo anaifanya kutetea wananchi wake na hasa kuboresha miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimwarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba tunavyozungumza hapa kwenye mgawo ambao umeishia awamu ya saba ya EP4R amepata mgawo wa shule mbili; Shule ya Kikunde mabweni mawili, matundu sita ya vyoo, vile vile na Shule ya Mafisa ambayo imepata madarasa manne na bweni moja na matundu sita ya vyoo.

Mheshimiwa Spika, vilevile swali lake la kwanza ni kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejitahidi sana, tumekarabati shule 45 kwa zile shilingi bilioni 60, lakini sasa tunaenda awamu ya pili, tunakarabati shule 17 kwa zaidi ya shilingi bilioni 17. Sasa shule aliyoitaja, tutaangalia kwenye orodha yetu, lakini tutaendelea kadiri itakavyowezekana. Ni nia ya Serikali kukarabati shule zote 89 hizi kongwe, zikamilike, lakini tumeanza zile ambazo tulizirithi kutoka kwa Wakoloni, ili tumalize twende na nyingine zote pamoja na hizi za kisasa ambazo wananchi wanachangia pia.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, naomba nimwarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba Mkutano huu ukimalizika tarehe 11 nitakuwa Tanga na Kilindi ni mojawapo. Tanga, Arusha na kuendelea. Kwa hiyo, niko tayari kutembelea shule hizi na kupata maelezo ya ziada. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)