Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ignas Aloyce Malocha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Primary Question

MHE. IGNAS A. MALOCHA aliuliza:- Serikali ilituthibitishia kuwa gesi aina ya Helium iligundulika katika Ziwa Rukwa na kwamba gesi hiyo ina thamani kubwa na ni adimu sana duniani:- Je, ni lini sasa Serikali itaanza kuchimba gesi hiyo ili Watanzania waanze kunufaika na gesi hiyo kabla haijagunduliwa au kuchimbwa mahali pengine duniani?

Supplementary Question 1

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Spika,
nashukuru kwa majibu mazuri na ufafanuzi wa swali langu la msingi umeeleweka lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza. La kwanza, ni lini Serikali itapeleka umeme wa REA III katika Jimbo la Kwela? Nauliza hivyo kwa vile Ukanda wa Ziwa Rukwa haujaguswa kabisa karibu Kata 13 na Kata saba za Ukanda wa Juu na zenyewe hazijaguswa kabisa, jumla Kata 20 hazijaguswa hata kijiji kimoja.
Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni lini Serikali itamalizia kupeleka umeme katika REA III katika vijiji 68 ambavyo havijapelekewa umeme katika Kata za Mpwapwa, Jangwani, Mpuhi, Likozi, Kalambanzite, Lusaka, Lahela na Sandurula?

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Malocha kwa jinsi anavyofuatilia masuala ya umeme kwa wananchi wa Jimbo lake. Mheshimiwa hongera sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini ni lini Serikali itapeleka
umeme katika Kata zake 20 ambazo zimebaki, kwanza kabisa tunakubaliana na Mheshimiwa Malocha kati ya Kata 27 zilizopata umeme ni Kata mbili ziko katika Jimbo lake. Kwa hiyo, Kata 25 zilizobaki kama ambavyo ameeleza ikijumlishwa pia Kata zake za Kipeta, Kilangawani, Kigamadutu pamoja na Malegesya na shule za sekondari
alizozitaja zitapatiwa umeme kupitia mradi wa REA ambao umeanza kutekelezwa nchi nzima mwezi huu.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimpe uhakika
Mheshimiwa Malocha kwamba Kata zake zote 27 na zile mbili ambazo zimepata bado Vitongoji vyake navyo vitapelekewa umeme kuanzia mwezi huu hadi miaka minne ijayo. Kwa hiyo, tuna uhakika Kata zako 27 Mheshimiwa Malocha zitakuwa zimepata umeme wa kutosha.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na vijiji 68, ni kweli
kabisa vipo vijiji 68 katika Jimbo la Mheshimiwa lakini na vitongoji 237. Tunapopeleka umeme katika vijiji 68 katika Jimbo la Kwela tunapeleka pia katika vijiji 237 ambapo vitongoji vyake vyote havijapata umeme.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa
Malocha vitongoji vyake vyote ambavyo havijapata umeme vile vya Mpwapwa, Muze, Halula na Mwandui vyote vitapata umeme. Ahsante sana.