Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 3 Sitting 41 Health and Social Welfare Wizari wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 348 2021-06-01

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza:-

Je, lini Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe itakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe?

Name

Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Japhet Ngailonga Hasunga, Mbunge wa Vwawa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe kwa kujenga majengo mawili ikiwa ni Jengo la Huduma za Uchunguzi wa Maabara ambalo limefikia asilimia 98 na Jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) ambalo ujenzi umefikia asilimia 96. Majengo haya mawili yanatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo mwezi Julai, 2021.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza ujenzi wa Jengo la Huduma za Afya ya Uzazi pale pale ambao utakamilika mwezi Februari, 2022 na kiasi cha shilingi bilioni tano kimetengwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.