Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 11 Sitting 60 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 506 2018-06-28

Name

Eng. Joel Makanyaga Mwaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chilonwa

Primary Question

MHE. ENG. JOEL M. MAKANYAGA aliuliza:-
Barabara inayounganisha Kata ya Haneti na Kata ya Segala kupitia Kata ya Zajilwa ni muhimu sana kwa kufungua mawasiliano katika kata hizo tatu:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kuwa barabara hiyo, inatengenezwa kwa kiwango cha kupitika muda wote kwa mwaka?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joel Mwaka Makanyaga, Mbunge wa Chilonwa, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha, 2017/2018 Serikali ilitenga na ilitoa fedha zote shilingi milioni 132.1 ambazo zimetumika kufanya matengenezo, si tu kwenye barabara aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge bali barabara ndefu zaidi ya kutoka Segala – Zajilwa – Haneti – hadi Umoja yenye urefu wa kilometa 80. Barabara hiyo, imekamilika na sasa inapitika muda wote wa mwaka.