Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 7 Sitting 46 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 374 2017-06-13

Name

Joram Ismael Hongoli

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupembe

Primary Question

MHE. JORAM I. HONGOLI aliuliza:-
Shule ya Sekondari ya Lupembe iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ni ya muda mrefu na tulishaomba na kufanya maandalizi ya kuwa na Kidato cha Tano kwa Mchepuo wa CBG.
Je, ni lini Serikali itaanzisha Kidato cha Tano katika
Shule hiyo?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joram Ismael Hongoli, Mbunge wa Lupembe, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Shule ya Sekondari ya Lupembe ni miongoni mwa shule mpya 22 ambazo zimeombewa kibali Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili iweze kupokea wanafunzi wa kidato cha tano katika mwaka 2017. Hivyo, shule hiyo itaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano baada ya kupatikana kwa kibali kilichoombwa kufuatia ukaguzi wa miundombinu ya shule iliyofanyika.