Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

Kuanzisha Mfuko wa Kulinda Ustawi wa Watoto Nchini Ni wajibu wa Serikali kulinda na kuhakikisha ustawi wa watoto katika nchi; Je, ni lini Serikali itatenga asilimia ya mapato yake katika bajeti ili kuwepo na Mfuko wa Kulinda Ustawi wa Watoto wa nchi hii?

Supplementary Question 1

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Napenda niulize maswali mawili tu ya nyongeza kwa Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Naibu Spika, mambo alioyasema Waziri nakubaliana nayo, lakini bado katika nchi yetu watoto wanaendelea kuteseka na wengine wanarandaranda mitaani. Je, Serikali haioni kwamba, imeshindwa kuweka maandalizi kwa ajili ya kutoa huduma sahihi kwa watoto? (Makofi)
Swali la pili, moja ya kazi za Serikali ni kuandaa kizazi chake kutoka kizazi kimoja hadi kingine na ndiyo maana nchi nyingine wanatenga mifuko kama hiyo na wanadiriki hata kulipa wanawake wanapokuwa wajawazito pesa kidogo kidogo ambazo baadaye umsaidia mzazi pale mambo yanapokuwa magumu kule mbele.
Je, sasa Serikali haioni ni wakti muafaka wa kufikiria kuanzisha mfuko huo ili kuweza kulinda watoto wetu wakue vizuri?

Name

Dr. Hamisi Andrea Kigwangalla

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, kuhusu mfuko, naomba arejee majibu yangu kwenye jibu la msingi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la kwanza, napenda tu kusema kwamba jukumu la malezi ni jukumu letu sote kama wazazi na linaanzia moja kwa moja kwenye familia. Sisi wanaume na wake zetu, tuchukue jukumu la kulea watoto tuliowazaa wenyewe. Kwa tamaduni za Kiafrika, extended family ina wajibu kwenye kulinda ustawi na kutoa ulinzi kwa watoto wote ambao wanaachwa na ndugu zetu, ambao pengine wametangulia mbele ya za haki ama wamepoteza uwezo wa kutoa malezi kwa mtoto.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo Wabunge ni Wajumbe, zina majukumu ya msingi ya kuhakikisha ulinzi na ustawi wa watoto kwenye maeneo yao. Hivyo, ninatoa wito kwa Wabunge wote na jamii kwa ujumla tuweke mikakati madhubuti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa tunakoishi kwa ajili ya kutoa ulinzi na ustawi kwa watoto.
NAIBU SPIKA: Waheshimiwa muda wetu umeenda sana. Tunaenda kwenye swali la mwisho, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, sasa aulize swali lake.