Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Upendo Furaha Peneza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. UPENDO F. PENEZA aliuliza:- Wananchi wa Mtaa wa Katoma, Kata ya Kalawala Wilaya ya Geita wameathirika sana na shughuli za Mgodi wa geita Gold Mine (GGM) ambapo nyumba zimepata nyufa na kuanguka kutokana na mitetemo, milipuko ya mara kwa mara inayoletwa na kelele na vumbi linaloathiri afya za wananchi wa mtaa huo pamoja na vyanzo vya maji. Je, ni lini wananchi hao wa Katoma watapewa fidia za mali zao ili waondoke katika eneo hilo jirani kupisha shughuli za Mgodi?

Supplementary Question 1

MHE. UPENDO F. PENEZA: Mheshimiwa Spika, tarehe 26 mwezi wa kwanza hapa Bungeni, Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, alitoa Kauli kwamba wananchi wengine wanashindwa kupata haki ya malipo stahiki kutokana na kitendo alichoita utegeaji. Kwamba wananchi wengine wanapanda wakati ule wanasubiri kwamba waweze kulipwa kwa wakati unaofuata. Sasa kutokana na hicho lakini naamini kwamba Mheshimwa Waziri, anafahamu ya kwamba wananchi huwa wanalipwa kutokana na asilimia ya ukuaji wa mmea husika, kwa hiyo kama mtu amepanda mgomba stahiki ni 50 kama mmea huo umekuwa kwa asilimia 10 basi utalipwa kwa asilimia hiyo 10. Je, kutokana na kauli hiyo ya Mheshimiwa Waziri, haoni kwamba Wizara hiyo itakuwa inashirikiana na migodi hiyo katika maeneo hayo ambako madini yanapatikana ili kuweza kuwanyima wananchi malipo stahiki kutokana na kazi yao katika maeneo yao husika?
Vilevile swali la pili, Geita ni sehemu ambayo inazungukwa na dhahabu kwa kiasi kikubwa, lakini katika maeneo mengine ambayo yameshalipwa fidia wananchi wamelipwa milioni moja na nusu kwa eka nzima, kwa maana ya fidia ya ardhi katika lile eneo. Lakini ukiangalia kwa maana ya wale wananchi hao hao wa Halmashauri hiyo ya Mji wa Geita, walipewa tena na Serikali kwa kuuziwa ardhi na kiwanja cha ishirini…
MHE. UPENDO F. PENEZA: Mheshimiwa Spika, najenga hoja. Kwa maana ya 25 kwa 30, wananchi hawa waliweza kununua eneo hilo hilo kwa milioni tatu. Maana yake ni kwamba ile milioni moja na nusu ambayo walilipwa haikuweza hata kutosha kununua heka nzima.
Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba wananchi wa maeneo ambayo yana madini waweze kulipwa malipo ya ardhi kulinganisha na bei ya soko iliyopo? Ahsante. (Makofi)

Name

Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Musoma Vijijini

Answer

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kauli yangu, naomba uelewe Mgodi wa Geita Gold Mine, watu wameanza kulipwa enzi ya plasadom, miaka ya 1980. Kwa hiyo huo mtegesho ni kweli na bahati nzuri tumepanga tarehe 10 mpaka 14, nakukaribisha na wewe uwepo Nyamongo kwa sababu nitakuwa na Mbunge wako hapa. Halafu hili suala la tathmini siyo kufikiria kwamba mtu anahitaji fedha kiasi gani ili akanunue shamba au akawekeze, anayefanya thathmini ni Ofisi ya Serikali na kila Wilaya inafanywa chini ya DC. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo sisi tunafuata taratibu za sheria ambazo zipo, tathmini siyo kukufanya wewe upate fedha kwa sababu umeshalenga mradi fulani. Ahsante.