Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Viwanja vya ndege nchini ukiondoa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere - Dar es Salaam havina miundombinu au huduma ya kubebea abiria wasiojiweza ikiwemo wagonjwa, wazee pamoja na watu wenye ulemavu. (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa huduma hii katika viwanja vingine nchini? (b) Huduma hii imekuwa ikifanya kazi na wakati mwingine kuharibika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere - Dar es Salaam, je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha huduma hii inapatikana muda wote kwenye uwanja huu wa Mwalimu Nyerere?

Supplementary Question 1

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ameelezea kwamba katika hivi viwanja vya ndege kuna wheel chairs na stretchers, lakini swali langu la msingi lilihoji kwa habari ya ambu-lift. Ukisema wheel chair inamsaidia tu yule mhitaji kumpeleka mpaka eneo la ndege, lakini anapofika pale inabidi abebwe juu juu na wale staff wa airport kitu ambacho kinakuwa ni very risk!
Mheshimiwa Naibu Waziri, kutokana na umuhimu wa ambu- lift, ni nini commitment ya Serikali kuhusiana na uwepo wa huduma hii katika viwanja vyote vya ndege nchini? Ahsante.

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana naye kwamba ambu-lift ndiyo kifaa kinachohitajika zaidi na chenye usalama zaidi kuliko hivyo vingine. Kama nilivyojibu katika jibu langu la nyongeza, Wizara yangu itahakikisha wale wanaotoa huduma kwa maana ya uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, tunawaongelea Swissport, na ninawataka Tanzania Airport Authority nao wahakikishe wanaongeza huduma hiyo ya ambu-lift katika kiwanja cha Mwalimu Julius Nyerere International Airport pamoja na Kilimanjaro, Songwe na viwanja vingine.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (WATU WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niseme natambua majibu mazuri ya Naibu Waziri wa Ujenzi. Niongezee tu mambo machache kuhusu huduma kwa watu wenye ulemavu katika viwanja vya ndege na maeneo mengine.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Sheria Na. 9 ya mwaka 2010 ilifuta sheria za zamani zilizokuwa zinazungumzia masuala ya watu wenye ulemavu, na moja ya mambo ambayo yameelezwa wazi katika sheria mpya hii ni kutambua suala la kufikika kirahisi na kupata huduma mbalimbali kirahisi kwa watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria hii ilianza kufanyakazi mwaka 2012 na ni wazi kwamba katika kipindi ambacho sheria hii imeanza kufanya kazi yapo, majengo na ipo miundombinu mingi sana ya Serikali ambayo kwa namna moja au kwa namna nyingine ilikuwa imejengwa kizamani.
Mheshimiwa Naibu Spika, commitment ya Serikali kuyabadilisha ipo, lakini hili ni suala ambalo litachukuwa muda na Ofisi ya Waziri Mkuu itakuwa inawasiliana na Wizara nyingine kadri inavyowezekana kuhakikisha kwamba taasisi zote za Serikali katika nyanja mbalimbali, elimu, afya, miuondombinu na kadhalika, zinachukuwa hatua zinazofaa ili kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanapata huduma stahiki, kokote wanakokwenda.

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Viwanja vya ndege nchini ukiondoa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere - Dar es Salaam havina miundombinu au huduma ya kubebea abiria wasiojiweza ikiwemo wagonjwa, wazee pamoja na watu wenye ulemavu. (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa huduma hii katika viwanja vingine nchini? (b) Huduma hii imekuwa ikifanya kazi na wakati mwingine kuharibika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere - Dar es Salaam, je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha huduma hii inapatikana muda wote kwenye uwanja huu wa Mwalimu Nyerere?

Supplementary Question 2

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ameelezea kwamba katika hivi viwanja vya ndege kuna wheel chairs na stretchers, lakini swali langu la msingi lilihoji kwa habari ya ambu-lift. Ukisema wheel chair inamsaidia tu yule mhitaji kumpeleka mpaka eneo la ndege, lakini anapofika pale inabidi abebwe juu juu na wale staff wa airport kitu ambacho kinakuwa ni very risk!
Mheshimiwa Naibu Waziri, kutokana na umuhimu wa ambu- lift, ni nini commitment ya Serikali kuhusiana na uwepo wa huduma hii katika viwanja vyote vya ndege nchini? Ahsante.

Name

Dr. Abdallah Saleh Possi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated