Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Primary Question

MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kusambaza Maji kutoka katika mradi wa Maji Kata za Miangalua na Mnokola katika Jimbo la Kwela? (b) Je, ni lini Serikali itapeleka Pesa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika maeneo hayo?

Supplementary Question 1

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Wizara, naomba kuuliza:-

Serikali ina mpango gani wa kutanua mradi wa maji wa Mji Mdogo wa wa Laela ili uweze kupeleka katika Kata ya Mnokola na Miangalua kwa sababu hivyo visima vimeshindwa kukidhi mahitaji ya wananchi katika Kata hizo?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Serikali inao Mpango wa kusambaza maji kutokana na vyanzo mbalimbali tulivyonavyo, na tutahakikisha tunafanya hivyo hivyo pamoja na chanzo hiki cha Rahela pia tutaenda kukifanyia kazi mwaka ujao wa fedha.