Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS (K.n.y. MWANTAKAJE HAJI JUMA) aliuliza:- (a) Je, ni lini Serikali itawapatia mtaji na kuwawezesha kiuchumi wananchi wengi ambao wamejiunga katika vikundi vya uvuvi? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia vifaa vya kisasa ili kuondokana na vifaa haramu?

Supplementary Question 1

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nina maswali mawili ya nyongeza madogo tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa adhabu hutolewa kwa wavuvi wanaovua kwa kutumia nyavu haramu. Je, kwa nini adhabu hiyo pia haiendi kwa yule anayemuuzia nyavu hizo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, ni lini Serikali itatoa elimu kwa wavuvi wetu ili na wao waweze kuvua kwa kuitumia bahari kuu ili iweze kuwanufaisha katika maisha yao? (Makofi)

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa fursa hii ya kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Fakharia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ametaka kujua kwa nini wale wanaowauzia na kuwasambazia wavuvi nyavu haramu hatuwachukulii hatua? Naomba nilihakikishie Bunge lako kwamba Wizara yetu imefanya kazi ya kuwachukulia hatua wote wanaouza na kusambaza na hata wanaozalisha nyavu hizo haramu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini juu ya suala la elimu, ni jambo endelevu, tumekuwa tukilifanya na tutaendelea kulifanya ili wavuvi wetu waweze kuendelea kunufaika na rasilimali zilizopo nchini.