Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hawa Mchafu Chakoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HAWA M. CHAKOMA (K.n.y. MARIA N. KANGOYE) aliuliza:- Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya matukio ya kikatili dhidi ya Watanzania wanaosafirishwa nje ya nchi na kufanyishwa kazi zisizo rasmi:- Je, Serikali imechukua hatua gani kudhibiti changamoto hii?

Supplementary Question 1

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, je, ni hatua gani kali na za kisheria zinazochukuliwa dhidi ya wafanyabiashara wanaosafirisha vijana wa Kitanzania hususan vijana wa kike kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanya biashara isiyo rasmi ikiwemo kuuza miili yao?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni ipi sasa kauli ya Serikali dhidi ya madai ya kusikitisha sana kuwa baadhi ya Watanzania wanasafirishwa kwenda nje ya nchi kuuzwa figo zao? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Susan Alphonce Kolimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza yaliyoulizwa na Mheshimiwa Hawa Mchafu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hatua gani kali za kisheria zimechukuliwa kwa wafanyabiashara ambao wamewapeleka wasichana nje na kwenda kufanya biashara ya kuuza miili yao, kwa kweli niseme tu kwamba kama taarifa hiyo ikijulikana hatua za kisheria za nchi yetu zitachukuliwa. So far mimi sina data za aina hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Watanzania ambao wamepelekwa nje na kwamba figo zinachukuliwa pia hiyo tutaifuatilia ili kama kuna ukweli, basi hatua kali zitachukuliwa kwenye nchi husika.