Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kiswaga Boniventura Destery

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Magu

Primary Question

MHE. KISWAGA B. DESTERY aliuliza:- Serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Magu fedha za ujenzi wa ofisi za halmashauri, lakini ujenzi huo haujakamilika:- Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo?

Supplementary Question 1

MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Kwa kuwa, mkandarasi anaendelea na mkataba mpaka kuezeka. Je, Serikali ina mpango gani wa ku-lease fedha ambazo zitahitajika, ili halmashauri isikiuke mkataba?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa, hatua ya kuezeka inakwenda kukamilika na jengo hili limechukua muda mrefu. Je, Serikali iko tayari kutenga fedha kwa mwaka ujao wa fedha, fedha za kutosha ili kukamilisha jengo hilo?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, kwanza ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba kandarasi zote ambazo zimeanzishwa hatuishii njiani. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie na nimwombe mkandarasi aliyepo hapo aendelee na kazi ili pesa ambayo imeahidiwa na Serikali ikifika asilazimike kwamba awe ametoka site na kulazimika kurudi kwa mara nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba kwa kushirikiana na Mbunge na nia njema ya Serikali kuhakikisha kwamba katika bajeti 2018/2019, ujenzi huu unaendelea, kwa hiyo tuweke kwenye bajeti.