Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Prosper Joseph Mbena

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. PROSPER J. MBENA aliuliza:- Ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda lililopo katika kata ya Serembala, Morogoro Kusini umesababisha matatizo makubwa kwa wananchi wa kata ya Serembala, Magogoni na vijiji jirani kutokana na fidia kidogo kwa kupisha ujenzi wa mradi huo ikilinganishwa na mali walizoziachia yaani mashamba, nyumba zao na mali nyingine zilizo kwenye maeneo makubwa ya ardhi iliyochukuliwa kwa ajili ya mradi huo. (a) Je, Serikali iko tayari kurudia zoezi la tathmini ya mali za wanavijiji wote walioathirika kwa kutoa nyumba na mashamba yao ili kupisha mradi wa bwawa la Kidunda na kuwalipa fidia wanayostahili? (b) Je, Serikali iko tayari kwenye bajeti hii kumalizia malipo ya takribani shilingi bilioni 3.7 kuwafidia wananchi hao kulingana na tathmini iliyofanyika? (c) Je, Serikali itakuwa tayari kuwawekea miundombinu ya uanzishwaji wa mashamba ya umwagiliaji na viwanda vidogo vidogo kwenye kata ya Serembala kwa ajili ya kutoa ajira kwa wananchi Serembala Magogoni, Mvuna na Kkata za jirani?

Supplementary Question 1

MHE. PROSPER J. MBENA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri, naomba kumuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.
Kwa kuwa fidia kamili kwa wale waliohusishwa na kuchukuliwa maeneo yao haijalipwa kama alivyozungumza Mheshimiwa Waziri kwamba kuna bakaa ya shilingi bilioni mbili ambayo wametenga kwa ajili ya kulipwa; na kwa kuwa, ninayo taarifa kwamba DAWASCO wameshapeleka mabango ili yawekwe kwenye maeneo yote ya sehemu hizo kuzuia wananchi wasifanye shughuli zozote za maendeleo, kwa maana kwamba tayari wameshakabidhiwa maeneo hayo.
Je, sasa Serikali iko tayari kusitisha uwekaji wa mabango hayo hadi wananchi watakapolipwa fidia yao kamili? (Makofi)
Swali la pili, kwa kuwa maeneo ya Bwakila Chini, Kiganila na Magogoni katika kata hii ya Serembala imekumbwa na mafuriko makubwa sana na wananchi wako kwenye maji kwa wiki tatu sasa.
Je, Serikali itapeleka msaada wa chakula na madawa ya dharura? (Makofi)

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa ni kweli tayari tumeshalipa zaidi ya shilingi bilioni saba katika hilo eneo na kilichojitokeza ni kwamba baada ya DAWASCO kulipa ile fedha yale maeneo kwa taarifa ambazo tulizipata wananchi walianza kuwauzia watu maeneo yale ambao hawajui kwamba maeneo yale yameshalipwa fidia. Baada ya taarifa hiyo kupatikana, Mkurugenzi wa Halmashauri yako Mheshimiwa Mbunge ndiye aliyeamua kuweka vibao ili kuweza kuwapa tahadhari wananchi kwamba lile eneo wasiuziwe kwa sababu lilishalipwa fidia vinginevyo tutapata matatizo zaidi katika Serikali. Kwa hiyo mabao yale niseme kwamba hayajawekwa na DAWASCO yamewekwa na Mkurugenzi wa Halmashauri yako.
Swala la mafuriko, kwanza nikupe pole kweli nami ninayo taarifa kwamba kuna baadhi ya vijiji ambavyo vimeingiliwa na maji, kwa vile taarifa hii uliyoitoa ya mafuriko na kuomba msaada Serikali imesikia na iko Idara husika inayohusika na jinsi ya kusaidia maeneo ya maafa basi nafikiri naomba ulifikishe huko ili liweze kushughulikiwa.