Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Salum Mwinyi Rehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Primary Question

MHE. SALUM MWINYI REHANI (K.n.y. MHE. MACHANO OTHMAN SAID) aliuliza:- Serikali yetu kwa muda imekuwa na uhusiano wa karibu na watu wa China, Serikali ya Watu wa China ina Ubalozi Dar es salaam na Ubalozi Mdogo huko Zanzibar:- (a) Je, Serikali haioni kuwa sasa umefika wakati wa kufungua Ubalozi Mdogo wa Tanzania katika Mji wa Guangzhou ili kutoa huduma nzuri kwa Watanzania wengi katika mji huo? (b) Je, ni utaratibu gani unatumika katika kuwapatia visa Watanzania ambao wameamua kuishi China zaidi ya mwaka mmoja.

Supplementary Question 1

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, lakini tulikuwa tunataka kujua mkakati gani Wizara inayo wa kuwafanya Wachina hawa kuhamisha teknolojia na viwanda ambavyo vinazalisha bidhaa mbalimbali kutoka kwao kule kuanzishwa katika nchi yetu?

Name

Dr. Susan Alphonce Kolimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati uliopo katika Wizara yetu na nchi ya China ni kufanya makubaliano na kusaini makubaliano hayo ya kuanzisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi Tanzania na China.