Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 3 Sitting 32 Good Governance Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu 257 2016-05-30

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Suala la Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma kwa muda mrefu limekuwa na kigugumizi na Ofisi za Wizara nyingi bado hazijahamia Dodoma, kutokana na kutokuwepo Sheria inayotamka kuwa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.
Je, ni lini Sheria hiyo itatungwa ili kuwezesha mchakato huo wa kuhamia Dodoma?

Name

Dr. Abdallah Saleh Possi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Fatma Hassan Toufiq, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeishaanza mchakato wa kutunga Sheria ya Makao Makuu ya Nchi. Tayari Waraka wa Baraza la Mawaziri wa kutunga Sheria hiyo umekamilika, na sasa unasubiri kupangiwa tarehe ya kujadiliwa katika kikao cha wataalam cha Makatibu Wakuu (IMTC) na kisha kuwasilishwa ngazi ya Baraza la Mawaziri kwa uamuzi na hatimaye kuandaliwa Muswada wa Sheria, utakaowekwa Bungeni kujadiliwa na kupitishwa na Bunge kuwa sheria.