Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 19 Sitting 4 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 30 2020-04-03

Name

Martin Alexander Mtonda Msuha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. MARTIN M. MSUHA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati Gereza Kuu Kitai lililopo Wilaya Mbinga?

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Martin Msuha, Mbunge Wa Mbinga Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Gereza Kuu Kitai ni miongoni mwa Magereza ya wazi lililojengwa kwa lengo la shughuli za kilimo na mifugo. Hata hivyo, Serikali inatambua tatizo la uchakavu hususani uzio wa Gereza uliozungushiwa kwa waya (Barbed Wire Fence) na nguzo za miti ambazo zimekuwa zikishambuliwa mara kwa mara na mdudu mchwa.

Mheshiwa Spika, katika kutambua tatizo la uchakavu huo, Serikali ina mpango wa kuyafanyia ukarabati mkubwa majengo na miundombinu ya magereza nchini likiwemo Gereza Kuu Kitai kwa kuzungushia Uzio kwa tofali na ukarabati wa mabweni ili kuboresha huduma za wafungwa na mahabusu.

Mheshimiwa Spika, aidha, ukarabati na uboreshaji wa miundombinu hiyo imepangwa kutekelezwa kwa awamu kwa kutegemea na upatikanaji wa rasilimali fedha.