Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 15 Sitting 45 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 379 2019-06-13

Name

Livingstone Joseph Lusinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtera

Primary Question

MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kituo kikubwa cha polisi katika Jimbo la Mtera hususani katika Kijiji cha Mvumi Misheni ili kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu katika Jimbo la Mtera?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Livingstone Lusinde, Mbunge wa Mtera kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, maeneo mengi ya vijijini nchini yameongezeka idadi ya watu, shughuli zao za kiuchumi na mambo mengine ambayo yanahitaji huduma ya ulinzi na usalama toka Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na Kijiji cha Mvumi Misheni.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Jeshi la Polisi inao mpango wa kuboresha na kujenga Vituo vya Polisi katika ngazi ya Tarafa na Kata nchi nzima ambavyo vitasaidia kusogeza huduma kwa wananchi hadi waliopo katika maeneo ya vijijini ikiwemo Kijiji cha Mvumi Misheni katika Jimbo la Mtera.