Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 14 Sitting 3 Policy, Coordination and Parliamentary Affairs Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu 26 2019-01-31

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:-

Kwa kuwa tumebakiza mwaka mmoja kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020 na ili Watanzania waliokidhi vigezo wapate haki ya kupiga kura, uboreshaji wa daftari la kupiga kura ni jambo lisiloepukika:-

Je, ni lini Serikali itaanzisha mchakato wa kuboresha daftari la wapiga kura?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, KAZI, AJIRA NA VIJANA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mchakato wa kuboresha Daftari la Wapigakura ulianza mwezi Agosti, 2018 kwa kufanya maandalizi yafuatayo:-

(i) Kuhuisha kanzidata ya Daftari la Kudumu la Wapiga kura; na

(ii) Kuboresha mifumo ya uandikishaji na utunzaji wa kumbukumbu za Daftari

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchuguzi ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mara ya kwanza na uandikishaji wa majaribio kwa baadhi ya mikoa ili kuona ufanisi au changamoto zinazoweza kujitokeza unatarajiwa kuanza hivi karibuni.