Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 11 Sitting 42 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 352 2018-06-01

Name

Lameck Okambo Airo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Primary Question

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO (K.n.y. MHE. LAMECK AIRO) aliuliza:-
Wilaya ya Rorya iliyoanzishwa mwaka 2007 sasa ina wakazi wapatao 400,000 na ina kata 26 na vijiji takriban 87 na ina vituo vya afya 4 lakini haina Hospitali ya Wilaya na wananchi wake hulazimika kutembea umbali wa takribani kilomita 30 kufuata huduma za afya Tarime na akina mama ambao ni asilimia 52 wanahitaji huduma ya hospitali kamili:-
Je, ni lini Wilaya ya Rorya itajengewa Hospitali ya Wilaya?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lameck Okambo Airo, Mbunge wa Rorya, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 105 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya 67 hapa nchini ikiwemo Hospitali ya Rorya ambayo tumeitengea shilingi bilioni 1.5.