Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 9 Sitting 5 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 67 2017-11-13

Name

Juma Selemani Nkamia

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. JUMA S. NKAMIA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya ya Chemba?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria napenda kujibu swali la Mheshimiwa Juma Suleimani Nkamia, Mbunge wa Chemba kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la Serikali ni kusogeza huduma karibu na wananchi. Juhudi kubwa zinaendelea kufanyika kuhakikisha kuwa kila Wilaya nchini inakuwa na mahakama. Katika mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali imepanga kujenga jingo la Mahakama Wilaya ya Chemba.