Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 7 Sitting 18 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 147 2017-05-05

Name

Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWANTUMU DAU HAJI aliuliza:-
Je, Serikali imejipangaje kuhusu huduma ya mabasi yaendayo kasi pale umeme unapokatika?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais - TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwantumu Dau Haji, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakala wa mabasi yaendayo haraka umejipanga vizuri kwa kuweka jenereta moja katika kila kituo kikubwa, ambalo hutumika kama chanzo cha umeme pale umeme wa TANESCO unapokatika. Vituo vikuu vilivyowekewa jenereta ni vya Kimara, Ubungo, Morocco, Kivukoni, Gerezani na katika karakana iliyopo Jangwani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pia kupitia DART imeweka betri za kutunza umeme (backup batteries) katika vituo vyote vidogo 27 ili zitumike kama chanzo cha umeme, pale umeme wa TANESCO unapokatika.